Nyumbani

Ibwe: Ibenge chachu ya mafanikio Azam

DAR ES SALAAM: UWEPO wa kocha Florent Ibenge umeongeza hamasa na morali ndani ya kikosi cha Azam FC kutokana na uzoefu na wasifu wake mkubwa katika soka la Afrika, jambo linaloaminika kuwa chachu ya kuimarisha ushindani wa timu hiyo katika mashindano mbalimbali.

Ofisa Habari wa Azam FC, Hasheem Ibwe amesema Dar es Salaam kuwa uwepo wa kocha huyo unawapa motisha viongozi, benchi la ufundi na wachezaji kuhakikisha wanatimiza matarajio yanayohusishwa na jina lake.

Amesema heshima ya kocha huyo ilidhihirika hata walipokwenda Casablanca, Morocco kucheza dhidi ya Wydad, ambako jina lake lilikuwa likitajwa kutokana na kazi nzuri aliyowahi kufanya akiwa RS Berkane.

“Kwetu sisi nafikiri inainua hamasa kwa viongozi na wachezaji kwamba huyu ni mwalimu mwenye CV kubwa. Tunapaswa kufanya kile ambacho watu wanakitarajia kutoka kwake ili kulinda heshima yake,” amesema.

Akizungumzia maandalizi ya timu katika kipindi cha mapumziko ya kalenda ya FIFA, Ibwe amesema wachezaji wamepewa mapumziko ya siku sita kabla ya kurejea kambini kuendelea na programu za mazoezi katika siku zilizobaki za mapumziko hayo ya takribani wiki tatu.

Amesema kipindi hicho kitawapa nafasi ya kuendelea kuimarisha kikosi huku wakizingatia mfumo wa mchezo na utambulisho wa timu ambao Ibenge ameujenga tangu kuanza kwa msimu.

“Kwa sasa timu imepewa mapumziko ya siku sita na baada ya hapo katika siku zilizobaki za wiki tatu, wachezaji watakuwa wamerejea uwanjani kuendelea kujitengeneza. Tunataka kuendelea na mfumo wa mchezo ambao mwalimu ameutengeneza kwa kikosi cha msimu huu,” amesema.
Mwisho

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button