Nyumbani

Oktoba ni zamu ya Barker na Mpanzu

DAR ES SALAAM: SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limemtangaza kiungo mshambuliaji wa Simba SC, Elie Mpanzu amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Oktoba wa Ligi Kuu Bara.

Mpanzu ameibuka mshindi dhidi ya lddi Selemani wa Azam FC na Nathaniel Chilambo wa Simba, alioingia nao fainali katika mchakato wa tuzo hizo.

Mchezaji huyo alitoa mchango mkubwa kwa timu yake katika michezo mitatu ambayo iliyocheza mwezi huo na kushinda yote, huku nyota huyo akifunga mabao matatu.

Naye kocha wa Wekundu hao, Steve Barker ameibuka kocha bora wa mwezi huo akiwazidi Florent Ibenge wa Azam na Juma Mgunda wa Namungo.

Barker aliiongoza Simba kushinda michezo yote mitatu iliyocheza mwezi huo na kupanda kutoka nafasi ya pili hadi ya kwanza kwenye msimamo wa Ligi Kuu.

Aidha, Kamati ya Tuzo ya TFF pia imeteua mabao matatu bora, ambayo yatapigiwa kura na mashabiki ili kupata bao bora la mwezi Oktoba.

Mabao hayo ni ya Hassan Mubiru (Azam v Mbeya City), Elie Mpanzu (Simba v Yanga) na Selemani Bwenzi (Simba v Mashujaa).

Kamati hiyo pia imemteua Meneja wa Uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Jackson Mwendwa kuwa Meneja Bora wa Uwanja kwa mwezi Oktoba kutokana na kufanya vizuri katika menejimenti ya matukio ya michezo pamoja na masuala yanayohusu miundombinu uwanjani.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button