Tetesi za usajili

LIVERPOOL inajiandaa na maisha baada ya winga Mohamed Salah, huku klabu hiyo ikitarajiwa kukubali kiasi kikubwa cha fedha kutoka klabu ya Ligi ya Kulipwa Saudi Arabia majira yajayo ya kiangazi. Mwaka huu Salah amekuwa mada kuu ya usajili kutoka timu ya Al-Ittihad.(CBS)
Kuhusu maingizo mapya Anfield, Kocha Jurgen Klopp anashinikiza Liverpool kumsajili beki wa kati wa Bayer Leverkusen, Piero Hincapie.(Fichajes)
Kocha wa Brentford ‘The Bees’, Thomas Frank amekiri kwamba The Bees ni ‘klabu ya kuuza’ na anafahamu kwa nini kuna nia kutoka timu nyingi kutaka kumsajili Ivan Toney. Arsenal na Chelsea ni miongoni mwa klabu zilizohusishwa na uhamisho wa mshambuliaji huyo katika wiki za hivi karibuni.(Sky Sports)
Chelsea na Bayern Munich zinafuatilia hali ya golikipa wa Arsenal, Aaron Ramsdale baada ya kutopangwa wakati mchezo The Gunners ilipopata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Everton Septemba 17, huku David Raya aliyesajiliwa majira ya kiangazi akichukua nafasi yake.(Daily Mail)
Manchester City inavutiwa kumsajili nahodha wa Chelsea Reece James, ambaye pia anahitajika Real Madrid.(Football Transfers)
Barcelona itakuwa na nafasi ya kumwangalia kwa karibu Arthur Vermeeren inayomwania wakati itakapoikabili Royal Antwerp katika mchezo Ligi ya Mabingwa Ulaya leo. Vermeeren mwenye umri wa miaka 18 anaonekana kuwa mbadala wa muda mrefu wa Sergio Busquets.(Gabriel Sans)
Golikipa wa zamani wa Manchester United, David de Gea anaweza kusajiliwa klabu mpya wiki hii, huku Real Betis ya Hispania ikipima uhamisho wa mchezaji huyo huru.(Fichajes)