Tetesi

Manchester United, Aston Villa zamwania Jonathan David

TETESI za usajili zinasema Manchester United na Aston Villa zina nia kumsajili fowadi raia wa Canada, Jonathan David, 23, anayekiwasha klabu ya Lille.(Football Transfers)

Kiungo mreno wa Liverpool Fabio Carvalho, 21, anatarajiwa kujiunga na timu ya Championship Hull City kwa mkopo kwa kipindi kilichobaki cha msimu huu. (Athletic – subscription required)

Mazungumzo yanaendelea kati ya Manchester City na Newcastle kuhusu kumsajili kiungo wa England, Kalvin Phillips, 28.(Rudy Galetti)

Wolves ina nia kumsajili fowadi mfaransa wa Paris Saint-Germain, Hugo Ekitike, 21. (L’Equipe – in French)

Related Articles

Back to top button