Ligi Kuu

Oura: Kila mchezo ni muhimu

DAR ES SALAAM: MSHAMBULIAJI wa Simba, Anicet Oura, amesema ataendelea kujituma kwa asilimia 100 ili kuisaidia timu hiyo kupata matokeo mazuri, akisisitiza kuwa kila mchezo ni muhimu katika safari yao ya msimu huu.

Oura amsema hayo baada ya Simba kuichapa Mashujaa mabao 6-1 jana, akieleza kufurahishwa na ushindi huo pamoja na kufanikiwa kufunga bao katika mchezo huo.

Amesema kikosi hicho kitaendelea kufanya kazi kwa bidii baada ya kupata ushindi katika mchezo uliopita dhidi ya Yanga, akisisitiza kuwa wanapaswa kuendeleza juhudi zao katika michezo inayofuata.

“Utukufu ni wa Mungu. Tunaendelea kufanya kazi kwa sababu kila mchezo ni muhimu. Tulishinda mchezo uliopita dhidi ya Yanga, hivyo tunaendelea na kazi yetu,” amesema Oura.

Ameongeza kuwa amefurahishwa na kufunga bao na kuona Simba ikiibuka na ushindi wa mabao 6-1, akieleza kuwa jukumu lake ni kufanya kazi kwa bidii ili kuisaidia timu.

Oura amesema ataendelea kuweka nguvu zake katika kuisaidia Simba, akiamini kuwa kujituma katika kila mchezo ni muhimu kwa timu hiyo kuendelea kupata matokeo mazuri.

Related Articles

Back to top button