Serie A
Osimhen: Nataka kuondoka Napoli

NAPOLI: MSHAMBULIAJI wa Napoli, Victor Osimhen ameomba kuondoka katika klabu hiyo ya Serie A, kwa mujibu wa mmoja wa wakurugenzi wake, Giovanni Manna.
Manna anakiri kwamba Osimhen angeweza kuwaacha mabingwa hao wa zamani wa Italia majira ya joto yaliyopita lakini alikwamba kutokana na kutopokea ofa kwa mshambuliaji huyo wa Nigeria.
“Victor Osimhen ameomba kuondoka kwenye klabu. Anataka kwenda,” Manna alisema.
“Hali iko wazi; tayari kulikuwa na nafasi za kuondoka kwake msimu wa joto uliopita. Victor anataka kuondoka. Tutaonana ndani ya siku 20 zijazo wapia anakenda.” Alisema Manna.
Napoli tayari wamekubaliana na mshambuliaji wa Chelsea, Romelu Lukaku kuchukua nafasi ya Osimhen kabla ya msimu mpya.