Okello: Nimefurahi kufungua akaunti ya mabao

SINGIDA: KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Allan Okello, ameeleza furaha yake baada ya kufunga bao lake la kwanza kwa timu hiyo katika ushindi wa mabao 3-0 walioupata dhidi ya Singida Black Stars.
Okello, ambaye alijiunga na Yanga katika dirisha dogo la usajili akitokea Vipers ya Uganda, alikuwa miongoni mwa wafungaji katika ushindi huo uliopatikana jana ugenini ikiwa ni mara ya kwanza anaifungia timu yake. Wengine waliofunga na Prince Dube na Mudathir Yahya.
Akizungumza baada ya mchezo huo, kiungo huyo alimshukuru Prince Dube, kwa msaada aliompa uwanjani pamoja na wachezaji wenzake waliomuwezesha kufunga bao hilo la kwanza akiwa na jezi ya Yanga.
“Namshukuru Dube kwa kunisapoti pamoja na wachezaji wenzangu. Ilikuwa ni kazi kubwa ya timu nzima kuhakikisha tunapata pointi tatu muhimu ugenini,” amesema Okello.
Mchezaji huyo ameahidi kuendelea kupambana ili kusaidia timu kupata matokeo mazuri katika michezo ijayo.
Pia, aliwashukuru mashabiki wa klabu hiyo maarufu kama Wananchi kwa kuendelea kuwapa sapoti katika kila mchezo.




