EPLKwinginekoSerie A

Ni suala la muda , Onana kutua United

KIPA Andre Onana anakaribia kujiunga na Manchester United, baada ya jana usiku Inter Milan na United kufikia makubaliano ya mwisho.

Imeelezwa mapema leo Julai 17, 2023 nyota huyo alifika kwenye kituo cha mazoezi cha Inter Milan na kuwaaga wachezaji wenzake kabla ya kusafiri kwenda Uingereza kukamilisha dili hilo.

kwa mujibu wa waandishi wa habari za michezo barani Ulaya  Onana  atasaini mkataba wa miaka mitano utakaomuweka Old Trafford hadi Juni 2028 wenye kipengele cha kuongeza mwaka mmoja.

Related Articles

Back to top button