Muziki

Kranium kuipeleka Dancehall ya Jamaica, Kenya

NAIROBI: MWANAMUZIKI nyota wa muziki wa dancehall kutoka Jamaica Kemar Donaldson maarufu kwa jina la Kranium amewasili nchini Kenya kwa ajili ya Onesho lake linalotarajiwa kufanyika Novemba 2 katika Ukumbi wa ASK Dome.

Mwimbaji huyo anayefahamika kwa wimbo wa ‘Ty Dollar’ amewasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) usiku wa kuamkia leo na kukaribishwa na waandaji wa onyesho hilo pamoja na washiriki kadhaa wa Dijitali ya Kenya.

Wimbo wa kwanza wa albamu, ‘Without You,’ aliomshirikisha Queen Naija, una vidokezo vya Afrobeat, dancehall reggae na R&B unatarajiwa kuburudisha mashabiki wake katika Onesho la ASK Dome lililoandaliwa na kampuni ya kimataifa ya burudani ya Airbeat.

Wasanii wengine watakaotumbuiza katika onesho hilo ni nyota wa muziki Redsan, Reedah, Mista C na Kaneda wote kutoka Kenya. Pia Joki maarufu diski au DJ Grauchi, ma DJ na MC wenzake akiwemo DJ Daffy, MC Gogo na Hype Ballo.

Akiwa na albamu yake mpya ya ‘In Too Deep’, Kranium atatumbuiza baadhi ya vibao vyake vinavyofahamika zaidi vikiwemo ‘Sidung’, ‘Nobody Has To Know’, ‘Gal Policy’ na ‘Toxic’.

Related Articles

Back to top button