Tennis

Murray ajitoa French Open

MWINGEREZA Andy Murray amejiondoa kwenye michuano ya French Open ili kuupa kipaumbele msimu wa ‘grass-court’ katika maandalizi ya Wimbledon.

Murray, 36, amecheza Roland Garros mara moja pekee tangu 2017.

Bingwa huyo mara tatu wa Grand Slam alishinda shindano la Clay-court Challenger huko Aix-en-Provence mwezi Mei.

French Open, Grand Slam ya pili ya mwaka, itafanyika kuanzia 28 Mei hadi 11 Juni.

Murray alishindwa na mpinzani wake wa muda mrefu Stan Wawrinka huko Bordeaux mapema wiki hii na pia aliondoka mapema katika hafla za ATP Tour huko Roma, Madrid na Monte Carlo.

 

 

Related Articles

Back to top button