Tennis

Gauff atinga raundi 4 French Open

NYOTA wa tenisi wa Marekani Coco Gauff leo ametinga raundi ya 4 ya French Open baada ya kumshinda Dayana Yastremska wa Ukraine kwa seti 6-2 6-4 licha ya kupata upinzani kutoka kwa raia huyo wa taifa la ulaya Mashariki.

Gauff, bingwa wa US Open sasa atakutana na mtaliano Elisabetta Cocciaretto hatua inayofuata.

“Niliwahi kucheza naye Madrid, na kwa kweli anacheza vizuri, hivyo nilidhani kumaliza mchezo inaweza kuwa vigumu kwa sababu alipiga vizuri baadhi ya mipira,” amesema Gauff wakati wa mahojiano uwanjani.

Coco Gauff anashika nafasi 3 kwa ubora wa mchezaji mmoja mmoja wa tenisi duniani.

Related Articles

Back to top button