Moallin kuvaa viatu vya Gamondi?

DAR ES SALAAM: KLABU ya Yanga imeachana na kocha Miguel Gamondi huku Abdihamid Moallin akitajwa kuchukuwa nafasi yake.
Taarifa kutoka kwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Yanga, Andre Mtine imesema kuwa wamevunja mkataba na kocha Gamondi na msaidizi wake Moussa Ndaw.
“Tunapenda kuwashukuru makocha hao kwa mchango wao ndani ya klabu na tunawatakia kila la kheri katika majukumu yao mapya,” amesema.
Mtine amesema mchakato wa haraka kutafuta makocha wapya wa kikosi cha Yanga umeanza na unatarajia kukamilika hivi karibuni.
Imeelezwa kuwa aliyekuwa kocha wa KMC FC, Moallin ameshamalizana na Yanga na tayari amesaini mkataba wa kukinoa kikosi cha timu hiyo.
Moallin ameachana na KMC FC baada ya mazoezo ya Jumanne ya Novemba 12 aliwaaga wachezaji na wasaidizi wake kuwa hatakuwa sehemu ya timu hiyo.
Alhamisi Novemba 14 KMC wametambulisha Kal Ongala kuwa kocha wa timu hiyo akichukuwa nafasi ya Moallin .