Kwingineko

Messi:Mpeno Lautaro hiyo Balon D’or

BUENOS AIRES: Nahodha wa timu ya taifa ya Argentina na Mshindi mara 8 wa tuzo ya mchezaji bora wa Dunia Balon D’or Lionel Messi amesema anaamini mshambuliaji wa Inter Milan, Muargentina mwenzake Lautaro Martinez anastahili kutwaa tuzo ya ya Balon D’or ya 2024.

Baada ya mchezo wa Jumanne usiku ambao Argentina iliitandika Bolivia kwa mabao 6-0, Messi na Lautaro Martinez wote wakiingia kambani Messi alisema umekuwa msimu mzuri kwa Martinez ambaye ameshinda Copa America na timu yake ya taifa, taji la Serie A akiwa na Inter Milan pamoja na kuchukua kiatu cha dhahabu cha Copa America akiwa na mabao matano hivyo haoni sababu ya mshambuliaji huyo kukosa Balon D’or.

 

“Amekuwa na mwaka mzuri sana, alifunga katika mechi ya fainali, alikua mfungaji bora Copa America, nadhani anastahili Balon D’or kuliko mtu yeyote” ,amesema Messi

Martinez ni mmoja wa nyota waliosalia katika orodha inayojumuisha nyota 30 wanaowania tuzo hiyo ambayo itatolewa usiku wa Oktoba 28 jijini Paris nchini Ufaransa na mshindi huyo mara 8 wa tuzo hiyo anaamini Lautaro ni mtu sahihi.

Tuzo hiyo yenye heshima kubwa Duniani itakuwa na mmiliki mpya mwaka huu huku majina ya nyota wanaosumbua kwa sasa ulimwenguni ni kama Erling Haaland, Phil Foden, Ruben Diaz na Rodri wa Manchester City, Jude Bellingham, Vinicius Jr na Kylian Mbappé wa Real Madrid, Lautaro Martinez Inter Milan pamoja na Bukayo Saka na Martin Odegaard kutoka Arsenal.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button