Man United yamwinda Todibo
TETESI za usajili zinaeleza kuwa Manchester United imemweka beki wa kati wa Nice na Ufaransa Jean-Clair Todibo kuwa kipaumbele chake kumsajili Januari 2024 huku mashetani hao wekundu wakiwa na nia kuboresha safu ya ulinzi.(Football Transfers)
Kwa upande wa wanaoondoka, wiki iliyopita Manchester United imewasiliana na Juventus kuhusu uwezekano wa dili kumtoa Jadon Sancho kwa mkopo. Klabu za Al Nassr na Al Hilal za Ligi ya Kulipwa Saudi Arabia pia zimeingia kwenye mbio kusaka saini ya winga huyo.(Daily Mail)
Kufuatia nia kama hiyo kutoka Saudi Arabia, Manchester United pia itafikiria ofa kwa ajili ya Casemiro Januari 2024. (TalkSPORT)
Chelsea imemweka Victor Osimhen kuwa mlengwa mkuu wa usajili wa mshambuliaji na anaaminika yupo tayari kuhamia Stamford Bridge lakini Napoli huenda wasimuuze Januari 2024 na hivyo The Blues kulazimika kusubiri hadi majira ya kiangazi. Chelsea pia inawania saini za Ivan Toney wa Brentford na Antonio Nusa wa Club Brugge.(Evening Standard)