Majeraha yasitisha huduma ya Diaz Man City

MANCHESTER: KOCHA mkuu wa mabingwa watetezi wa ligi kuu ya England Manchester city Pep Guardiola amesema beki wake Mreno Ruben Diaz atakuwa nje kwa wiki nne kufuatia jeraha alilopata katika mchezo wa dabi ya Manchester wikiendi iliyopita.
Beki huyo alikosa michezo yote ya Novemba kutokana na majeraha kwenye mguu wake wa kulia lakini akarejea mwanzoni mwa mwezi Desemba lakini Guardiola anasema beki huyo atakuwa nje kuanzia mchezo wa kesho dhidi ya Aston Villa ugenini Villa park.
“Ruben tutamkosa tena kwa muda mrefu. Alicheza dakika 75 dhidi ya Manchester United na alijihisi maumivu lakini ni mvumilivu sana aliendelea kubaki uwanjani” – Amesema Guardiola
Manchester City wanaendelea kuandamwa na majeraha msimu huu huku eneo lao la ulinzi likiwa ndilo lililoathirika sana. Kesho watarudi uwanjani kujaribu tena kuwapa furaha mashabiki wa timu hiyo ambao wamekuwa kwenye mashaka kwa muda mrefu.