Liverpool yataka saini ya Éderson
TETESI za usajili zinasema Liverpool inajiandaa kuanza mchakato kumsajili kiungo mkabaji Éderson José dos Santos Lourenço da Silva, ‘Éderson’ wa Atalanta katika kile kinachoweza uwa uasajili a kwanza wa kocha mpya wa The Red, Arne Slot.
Éderson alikuwa na msimu bora Atalanta, akifunga mabao 6 na kutoa pasi 1 ya bao katika michezo 35.
Amecheza mechi 52 katika mashindano yote ya kikosi bingwa cha Kombe la Ligi ya Europa cha kocha Gian Piero Gasperini akionesha kiwango kilichomfanya kuitwa timu ya taifa ya Brazil kwa ajili ya michuano ijayo ya Copa America.
Éderson ana miaka 3 imebaki katika mkataba wake Atalanta lakini inaonekana kama ofa za usajili toka Premier League zinaibuka tena baada ya kuhusishwa na Newcastle United na Tottenham Hotspur Januari, 2024.