Tetesi

Liverpool sasa yageukia kwa Ruben Amorim

TETESI za usajili zinasema mlengwa aliyependekezwa katika timu ya Liverpool kumrithi Jurgen Klopp kuwa kocha wa klabu hiyo ajaye ni bosi wa Sporting Lisbon mreno Ruben Amorim, baada ya Xabi Alonso kutangaza kubaki Bayer Leverkusen. (Liverpool Echo)

Amorim, 39, ana kipengele cha kuachiwa cha pauni mil 12.8 kitakachoanza mwisho wa msimu. (Telegraph – subscription required)

Matumaini ya Barcelona kumsajili winga wa Palmeiras ya Brazil, Messinho,16, yanaongezeka lakini Manchester City, Manchester United, Chelsea, Arsenal na Paris St-Germain pia zinahusishwa na mbrazili huyo. (Mundo Deportivo – in Spanish)

Liverpool imeonesha nia kuhitaji huduma ya winga wa Eintracht Frankfurt na Misri Omar Marmoush, 25, iwapo mmisri mwenzake Mohamed Salah, 31, ataondoka Anfield majira yajayo ya kiangazi. (Mundo Deportivo – in Spanish)

Manchester United inaweza kuhuisha kipengele cha kuachiwa cha pauni mil 51.3 kumsajili beki wa Brazil, Gleison Bremer, 27, toka Juventus. (Repubblica – in Italian)

Related Articles

Back to top button