Nyumbani
Ligi ya Mabingwa mikoa Machi 10

LIGI ya Mabingwa wa Mikoa(RCL2023) hatua ya makundi inatarajiwa kuanza Machi 10, 2023.
Taarifa ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) imevitaja vituo vya ligi hiyo itakayokuwa na timu saba kila kituo zitakazocheza ligi ya mkondo mmoja kuwa ni Kagera, Kigoma, Shinyanga na Katavi
Timu kwa kundi la ligi hiyo ni kama ifuatavyo:
Kundi A: Kagera
Buhaya, Shilabela, Mapinduzi, Nyamongo, Damali, Nyumbu na Eagle.
Kundi B: Kigoma
Aglo Sports Academy, Mambali Ushirikiano, Singida Cluster, Arusha City, Tanesco, Kiluvya, na Kilosa United.
Kundi C: Shinyanga
Maila Boys, Bus Stand, Aca Eagle, Eagle Rangers, Mbuga na Navy.
Kundi D: Katavi
Malimao, THB, Hollwood, KFC, Ilula Tigers, Zamalek na Mbinga United.