Mmemsikia Dube?

DAR ES SALAAM: MSHAMBULIAJI wa Yanga, Prince Dube amesema hana mpango wa kuingia katika mbio za kuwania ufungaji bora kwa msimu huu.
Amesema anachozingatia kwa sasa ni kuisaidia timu yake kupata alama tatu katika kila mechi ili kufikia malengo ya kutetea taji la ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
“Ufungaji bora bado nataka kusaidia timu yangu kushinda na kuvuna alama tatu kila mechi tusonge mbele, suala ufungaji bora litakuja baadae sana kwa sababu kuna washambuliaji wazuri wanafunga kila siku,” amesema.
Dube ameongeza kuwa akili na nguvu zake anazielekeza zaidi kuona klabu yake inapata mafanikio ikiwemo kutetea taji la ubingwa na kufanya vizuri katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Dube amefunga Hat trick ya kwanza jana katika Ligi katika mchezo dhidi ya Mashujaa FC, uwanja wa KMC Complex uliopo Mwenge.