Ligi KuuNyumbani

Makocha Yanga, Simba kitete Ngao ya Jamii

WAKATI joto la fainali ya Ngao ya Jamii kati ya Yanga na Simba Agosti 13 likizidi kupanda, makocha wa timu hizo wametambiana kila moja timu yake kushinda mchezo huo wa watani wa jadi.

Wametoa tambo hizo jijini Tanga leo wakati wakizungumza na waandishi wa habari kuelekea kipute hicho kwenye uwanja wa Mkwakwani.

Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amesema mchezo utakuwa mkubwa na mzuri kwa klabu yake hasa kwa mwanzo wa msimu na anajua umuhimu wa mchezo huo kwa kila timu.

“Ni Furaha kwangu kucheza mchezo huu mkubwa kesho, matarajio yetu ni kufanya vizuri na tumejiandaa bila presha yoyote kwasababu nimeshakutana na michezo ya aina hii mingi, tunaenda kupambana kwa ajili ya nembo ya Young Africans SC na Mashabiki wetu ambao wapo nasi kiła siku,” amesema Gamondi.

Kocha Mkuu wa Simba, Robertinho Oliveira.

Naye Kocha Mkuu wa Simba Robertinho Oliveira amesema pamoja na ugumu wa mchezo huo klabu yake ipo tayari kushinda.

“Derby ni Derby na siku zote haitabiriki. Tunafahamu itakuwa mechi ngumu na tunaiheshimu Yanga lakini tupo tayari kuhakikisha tunashinda,” amesema Robertinho.

Kufika fainali Yanga imetoa Azam kwa mabao 2-0 wakati Simba imeondoa Singida Fountain Gate kwa mikwaju ya penalti 4-2.

Related Articles

Back to top button