Nyumbani
KMC yaivutia kasi Ligi Kuu

WAKATI Ligi Kuu Tanzania Bara imesimama kupisha michuano ya kimataifa, klabu mbalimbali zimeendelea kujiweka sawa kwa ajili ya mashindano mbalimbali.
Katika maandalizi hayo KMC leo imecheza mechi ya kirafiki dhidi ya timu ya Ngome kwenye uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam na kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.
“Lengo ni kujiweka sawa na michezo ya ligi mwezi huu,” imesema KMC.
Kwa mujibu wa ratiba mchezo unafuata wa KMC ligi kuu utafanyika Septemba 15 dhidi ya JKT Tanzania.