Nyumbani

Tuzo za TFF kutolea Ngao ya Jamii

TUZO za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) sasa zitakuwa zikifanyika wakati wa michezo ya Ngao ya Jamii.

Taarifa ya TFF imesema lengo la mabadiliko ya hafla hizo za kuwatuza wachezaji bora wa msimu ni kufanya maboresho ya kulifanya tukio kuwa bora zaidi kukidhi malengo na mahitaji yake.

“Kwa mabadiliko hayo halfa ya Tuzo za TFF kwa msimu wa 2023/2024 itafanyika wakati wa michezo ya Ngao ya Jamii kufungua msimu wa 2024/2025,” imesema taarifa.

Tuzo hizo hutolewa kwa wanamichezo waliofanya vizuri katika mashindano yanayoandaliwa na TFF, Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB) na matukio mengine rasmi yenye kuambatana na mpira wa miguu hapa nchini.

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button