Karia:Klabu tafuteni stadi za uongozi

DAR ES SALAAM: Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania Wallace Karia amewataka viongozi wanaoendesha klabu kuhakikisha wasome stadi za uongozi kuondokana na anguko kwenye mpira wa miguu.
Karia ameyasema hayo Dar es Salaam leo wakati akizungumza na wahitimu wa mafunzo ya soka la ufukweni ambao ni maofisa wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Amesema kuna watu wakipewa mipira huko wanapewa uongozi kwenye klabu wanawasumbua hivyo, inabidi wafanye kozi za ustadi za uongozi kuepusha anguko linaloweza kutokea mbele la mpira wa miguu.
“Tufanye kozi tupate ujuzi ili tuendeshe klabu zetu kwa weledi na maadili yanayotakiwa la sivyo yale mafanikio tunayopata yanaweza kuwa anguko,”amesema.
“Kiongozi kama huwezi kusimama kama kiongozi unaweza kupelekea anguko kwenye ligi, klabu na mpira wa miguu,”amesema.
Amesema mafanikio yanayoonekana kwa baadhi yao wamepitia mafunzo mbalimbali ya uongozi.