Africa

Kama mlivyosikia Yanga unajipigia tu

DAR ES SALAAM: Yanga wamepoteza mabao 2-0 mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Hilal wakiwa nyumbani Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Bao la kwanza Al Hilal limefungwa dakika ya 65  na Adama Coulibali baada ya kumpiga chega beki wa Yanga, Ibrahim Hamad na kipa Djigui Diarra mpira kuingia nyavu.Yasir Mozamil amefunga bao la pili Al Hilal dakika ya 90 ya mchezo.

Hii ni mechi ya tatu mfululizo kupoteza walianza na Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Azam FC na Tabora United wakiwa nyumbani uwanja wa Azam Complex ,leo mechi ya tatu na Al Hilal ya Sudan.

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button