Africa

Yanga yatanguliza mguu moja makundi

KLABU ya Yanga imeanza vizuri katika mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya kwanza kwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya CBE SA ya Ethiopia, mchezo uliochezwa Uwanja wa Abebe Bikila, Addis Ababa.

Bao la Yanga kwenye mchezo huo ilifungwa na Prince Dube.Licha ya kufunga bao hilo Dube amepoteza nafasi nyingi za wazi ambazo zingeweza kubadilisha matokeo zaidi.

Dakika ya 45 kipindi cha kwanza , timu zote zilicheza vizuri Yanga walifanikiwa kufika langoni kwa mpinzani mara kwa mara.

Mashambulizi ya Yanga, ndani ya dakika 40 ya kipindi cha kwanza Dube ameshindwa kutumia nafasi nyingi kabla ya kufunga bao hilo pekee lililowapa ushindi.

Dakika 72 Clement Mzize alikosa nafasi ya wazi akipokea pasi kutoka Pacome Zouzoua, Clatous Chama naye alishindwa kufunga dakika ya 90 baada ya kupokea pasi maridhawa kutoka kwa Clement Mzize.

Yanga sasa wanatarajiwa kurejea nchini na kujiandaa na mchezo wa mkondo wa pili ambao ndio utakaoamua timu itakayocheza hatua ya makundi ya michuano hiyo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button