EPLKwingineko

Joelinton nje wiki sita

KIUNGO wa Newcastle United ‘The Magpies’, Joelinton Cássio Apolinário de Lira (Joelinton) atakaa nje ya uwanja kwa muda usiopungua wiki sita baada ya kupata jeraha la paja.

Joelinton, 27, amepata jeraha hilo Januari 6 wakati wa mchezo wa Kombe la FA, The Magpies iliposhinda mabao 3-0 dhidi Sunderland.

Akizungumza leo Kocha wa Newcastle Eddie Howe amesema: “Joelinton ni kiungo kiongozi, ni pigo kubwa kwetu kumkosa.”

Kikosi cha Howe kimekumbwa na idadi kubwa ya majeruhi kwa sasa msimu huu huku Joelinton akiwa wa 11.

Newcastle itaikaribisha Manchester City kwenye uwanja wa St. James Park Januari 13 katika mchezo wa Ligi Kuu England.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button