Ligi Daraja La Kwanza
Job afanyiwa upasuaji, Rais Hersi amtia moyo

DAR ES SALAAM: Nahodha Msaidizi wa Yanga, Dickson Job, amefanyiwa upasuaji wa goti nchini Afrika Kusini kufuatia majeraha aliyoyapata katika mchezo wa Kariakoo Dabi dhidi ya Simba uliochezwa Machi 1, 2026.
Job alipata majeraha hayo katika kipindi cha kwanza baada ya kugongana na kiungo wa Simba, Inno Loemba wakati wakigombea mpira, hali iliyomlazimu kutolewa uwanjani na kushindwa kuendelea na mchezo huo.
Uongozi wa klabu hiyo pia umemtumia ujumbe wa kumtakia nafuu ya haraka mchezaji huyo ambaye alikuwa tegemeo kwenye kikosi cha kwanza.
Rais wa Yanga, Hersi Said, amesema wana imani beki huyo atarejea akiwa na nguvu zaidi.
“Utarudi ukiwa imara kuliko ulivyokuwa awali,” amesema Hersi kupitia mtandao wa Yanga.




