Ligi Kuu

JKT Tanzania yaomba radhi jeraha ya Pacome

DAR ES SALAAM: UONGOZI wa Klabu ya JKT Tanzania umeomba radhi kufuatia kuumia kwa kiungo wa Yanga SC, Pacome Zouzoua, katika mchezo wa kuhitimisha msimu wa 2025/26 wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa Juni 30, 2026 kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Dar es Salaam.

Pacome alipata jeraha baada ya kugongana na mchezaji wa JKT Tanzania, Hassan Wahabi, wakati wakiwania mpira katika mchezo huo.

Kupitia taarifa yake, JKT Tanzania imesema tukio hilo halikuwa la makusudi na kwa niaba ya Hassan Wahabi, uongozi wa klabu hiyo umeomba radhi kwa maumivu aliyoyapata nyota huyo wa Yanga.

Klabu hiyo imeeleza kuwa Wahabi naye ameguswa na tukio hilo na hakukusudia wala hakutarajia kumsababishia majeraha Pacome.

Mbali na kuomba radhi, JKT Tanzania imemtakia Pacome nafuu ya haraka na kumuombea apone mapema ili arejee uwanjani kuendelea kuonesha kiwango chake.

Related Articles

Back to top button