Ligi Kuu

Yanga yaishusha Simba kileleni

DAR ES SALAAM: KLABU ya  Yanga imekwea kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara baada ya kuibuka  na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Kagera Sugar.

Ushindi huo umeifanya Yanga kufikisha alama 42  kupanda  kileleni mwa  msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa mara ya kwanza.

Bao  la kwanza la Yanga limefungwa na Clement Mzize shuti dakika ya 32 akiunganisha mpira wa pasi  iliyopigwa na Stephane Aziz Ki. Mudathir Yahya aliiongezea bao la pili Yanga dakika ya 60 kazi nzuri iliyofanywa na Prince Dube. Pacome Zouzoua aliipatia Yanga bao la tatu dakika 78 kwa mkwaju wa penalti ya baada ya Max Nzengeli kukwatuliwa na Datius Peter  na mwamuzi Nassoro Mwinchui kufunika mkwaju wa penalti.

Mtokea benchi Kennedy Musonda aliipatia timu yake bao la nne dakika ya 86 na kuhitimisha ushindi wa mabao 4-0.

Aziz Ki amekosa penalti dakika ya 35 amepiga shuti lakini kipa wa Kagera Sugar Ramadhani Chalamanda aliucheza mpira .

Kwa matokeo hayo Yanga imeishusha Simba kwenye msimamo hadi nafasi ya pili akiwa na alama 40 na kesho anashuka dimba la Al Hassan Mwinyi, Tabora dhidi ya Tabora United.

Related Articles

Back to top button