Filamu

James Cameron kuja na filamu ya bomu la Hiroshima

HOLLYWOOD: Muongozaji wa filamu ya Titanic, Avata 1 &2 na filamu nyingine nyingi zilizofanya vizuri katika mauzo duniani, James Cameron ametangaza kufanya majaribio ya mwisho kwa ajili ya kutengeneza filamu inayohusu kulipuliwa kwa mji wa Hiroshima mnamo Agosti 6, 1945.

Cameron amesema kama hakutakuwa na changamoto za zuio la filamu hiyo atafurahi kuikamilisha kwa kuwa amekuwa akitamani kufanya filamu hiyo kwa miaka mingi.

Muongozaji huyo licha ya kuwa katika hatua ya mwisho za maandalizi ya filamu ya Avata 3 &4 amesema hazita mzuia kukamilisha filamu ya Hiroshima atakayoiita ‘Last Train from Hiroshima’.

Katika kuhakikisha anafanikisha hilo, Cameron amenunua haki za kitabu cha Charles Pellegrino cha 2015, ‘Last Train from Hiroshima’, na amepata haki za ufuatiliaji wa mwandishi wa ‘Ghosts of Hiroshima’.

Filamu hii ikikamilika itakuwa filamu ya kwanza ya muongozaji huyo isiyo na mfumo wa Avatar tangu alipotoa filamu ya Titanic mwaka 1997 hakutoa filam u nyingine kama hiyo hadi leo.

Cameroon, “Siku chache kabla ya kifo cha muhusika mkubwa eneo la Hiroshima na Nagasaki, Tsutomu Yamaguchi nilikutana naye akiwa hospitalini na alinihadithia kuhusu eneo la Hiroshima hivyo siwezi kuepuka kuifanya filamu hiyo,”

Katika hatua nyingine muongozaji huyo baada ya kutoa filamu ya Avatar 3 &4 amepanga kutoa Avatar 5 kabla ya mwaka 2031 filamu ambayo amesema itaonyesha mwisho wa muongozaji huyo katika uongozaji wa filamu

Related Articles

Back to top button