Kwingineko

Huu ndiyo uamuzi wa Uingereza dhidi ya Harry Maguire

LONDON, England

BEKI Harry Maguire anatarajiwa kuanza katika mchezo wa UEFA Nations League utakaopigwa leo jioni ugenini huko Jamhuri ya Ireland.

Mchezo huo utapigwa katika Uwanja wa Aviva mjini Dublin ikiwa ni mechi ya kwanza chini ya meneja wa muda Lee Carsley.

Maguire alikuwepo katika mafanikio ya Gareth Southgate, lakini jeraha lilimfanya ashindwe kushiriki Euro 2024 michuano ya kwanza ya kimataifa ambayo hakushiriki tangu acheze kwa mara ya kwanza mwaka 2017.

Gazeti la The Mirror linaripoti kwamba Maguire yuko tayari kuanza dhidi ya Ireland na Carsley hana tatizo na Maguire huku akimsifia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 kwenye mkutano wake na waandishi wa habari kabla ya mechi.

“Yeye ni kiongozi,” Carsley alisema kuhusu Maguire. “Anaongoza kwa mfano katika maandalizi yake ndani na nje ya uwanja.

“Katika mechi ambazo nimemwona akicheza, nadhani amekuwa na nguvu zaidi kadri michezo inavyoendelea. Ni wazi, hakucheza katika mechi ya mwisho ya Manchester United, lakini aliingia kambini vizuri sana.

“Na kiakili, ndio, amekuwa mzuri ndani na nje ya uwanja nilihisi. Ninachotaka tayari tumekuwa nacho kuhusiana na jinsi amekuwa karibu na kikosi yupo vizuri.”

Maguire alianza mechi mbili za kwanza za United kwenye kampeni za Ligi Kuu, ushindi wa 1-0 dhidi ya Fulham na kupoteza 2-1 dhidi ya Brighton & Hove Albion, ingawa aliondolewa katika hatua za mwisho za mechi zote mbili ili kudhibiti utimamu wake.

Kisha aliingia akitokea benchi kwenye mechi waliyochapwa 3-0 nyumbani na wapinzani wao Liverpool wikiendi iliyopita.

Related Articles

Back to top button