Thierry Henry abwaga manyanga Timu ya taifa Ufaransa

PARIS: MCHEZAJI wa zamani wa Arsenal na timu ya taifa ya Ufaransa, Thierry Henry ameacha kuifundisha timu ya vijana wa chini ya miaka 21 wa Ufaransa baada ya kushindwa na Uhispania katika fainali ya Olimpiki huku akidai ameamua kuachia ngazi kwa sababu zake mwenyewe.
Gwiji huyo wa Arsenal aliteuliwa kushika nafasi hiyo Agosti mwaka jana baada ya kuinoa Ubelgiji, Monaco na Montreal Impact.
Alifanikiwa kuiongoza timu hiyo kutwaa medali ya fedha ya kuvutia, na kukosa dhahabu kwa Uhispania ambao waliwashinda 5-3 baada ya muda wa nyongeza kwa mabao mawili ya mwisho ya Sergio Camello.
Na sasa Henry ameacha kazi hiyo baada ya chini ya mwaka mmoja na kufichua kuwa ‘sababu zake mwenyewe’ ndizo zilichangia uamuzi huo.
Henry alicheza kwa mafanikio akiwa Arsenal na timu ya taifa ya Ufaransa.