Bundesliga

Hatma ya Dortmund mikononi mwa Bayern

BERLIN, Wanafainali wa Ligi ya mabingwa msimu uliopita Borussia Dortmund sasa watajua hatma yao ya michuano ya UCLmsimu ujao kwenye mchezo wa Dabi ya Ujerumani maarufu kama Der Klassiker baada ya kuchakazwa 4-0 na Barcelona kwenye UCL usiku wa kuamkia leo na kufifiza matumaini ya kufuzu kupitia kuwa mabingwa.

Dortmund ambao wanaonekana kuhitaji maandalizi makubwa ndani ya muda mchache walionao watasafiri hadi Allianz Arena kuwavaa vinara wa ligi hiyo Bayern Munich jumamosi hii ya Aprili 12 kuanzia majira ya saa 1:30 usiku Afrika Mashariki.

Kibarua cha kocha Niko Kovac kinazidishwa ugumu na kukosekana kwa mmoja wa wachezaji muhimu wa kikosi hicho beki Nico Schlotterbeck ambaye hatapatikana msimu huu kutokana majeraha.

Dortmund wapo nafasi ya 8 kwenye msimamo wa Bundesliga na pointi 41, pointi 5 nje ya eneo la ‘top 4’ wanakopaswa kuwa ili wafuzu moja kwa moja kwa msimu ujao wa Ligi ya Mabingwa na tayari viongozi wa klabu hiyo wana wasiwasi itashindwa kufuzu katika michuano yeyote ya Ulaya msimu ujao licha ya hakikisho kutoka kwa kocha Kovac kuwa inawezekana.

Related Articles

Back to top button