Masumbwi

Faru Weusi uso kwa uso na Nigeria, Zambia

GLASGOW: TIMU ya Taifa ya Ngumi ya Tanzania maarufu kama Faru Weusi imepangiwa kuanza kampeni yake dhidi ya wapinzani kutoka Nigeria, Zambia na Lesotho katika michezo ya Jumuiya ya Madola inayofanyika nchini Scotland.

Katika uzani wa Light Heavyweight (kg 80) hatua ya 32 bora, Yusuf Changalawe ataanza safari yake kwa kupambana na Ankintola David kutoka Nigeria. Naye Faki Issa atashuka ulingoni hatua ya 32 bora katika uzani wa Bantamweight (kg 55) dhidi ya Mwengo Mwale kutoka Zambia.

Kwa upande wa wanawake, Zawadi Kutaka maarufu kama “Tanzanite Queen”, ambaye ni mwanamke wa kwanza kuiwakilisha Tanzania katika mchezo wa ngumi kwenye Michezo ya Jumuiya ya Madola, ameanza kwa mafanikio baada ya kufuzu moja kwa moja hatua ya robo.

Zawadi atamenyana na bondia kutoka Lesotho katika uzani wa Featherweight (kg 57).

Kwa upande wa ngumi, michezo itaanza rasmi kesho Ijumaa, tarehe 24 Julai 2026, katika ukumbi wa Scottish Event Campus (SEC), Glasgow, Scotland.

Jumla ya mabondia 201 (131 Wanaume, 70 Wanawake) kutoka mataifa 43 wanatarajiwa kushiriki katika uzani 14 (uzani saba za wanaume na saba za wanawake)

Related Articles

Back to top button