EPL

Ederson: usajili mpya umetubusti

MANCHESTER, GOLIKIPA wa Manchester City Ederson Morales amesema usajili uliofanyika klabuni hapo mwezi Januari umewasogeza hatua moja kuelekea kwenye kurejesha ubora waliokuwa nao awali baada ya kuonekana kupoteana msimu huu.

Mbrazil huyo amesema imani yake ni kuwa kadri siku zinavyokwenda usajili wa wachezaji hao utalipa na Manchester City itarejea kwenye ubora wake ambao umeifanya klabu hiyo kutawala soka la England kwa misimu minne mfululizo.

Mabingwa hao watetezi wa ligi kuu ya England mwezi Januari walifanya usajili wa wachezaji watano ambao ni mshambuliaji Omar Marmoush kutoka Frankfurt, beki wa kati Abdukodir Khusanov kutoka RC Lens, kiungo Nico Gonzales kutoka FC Porto, kiungo mshambuliaji Claudio Echeverri kutoka River Plate ya Argentina na beki wa kati wa Brazil Vitor Reis.

“Wametusaidia sana, kwa kipindi kile tulichokuwa na majeruhi wengi kwenye kikosi naona ujio wao ni wa maana sana. Khusanov anacheza vizuri sana, Nico pia alikuja kwenye kipindi tulichomhitaji sana. Vitor Reis ni kipaji kipya kwenye kikosi namuona mbali sana”

“Omar naona amekuja kuichachua safu ya ushambulizi na ametusaidia sana kuwa na nguvu ya kuifungua ngome ya timu pinzani. Kwakweli nafurahia uwepo wao pamoja na Echeverri ambaye amewasili hivi karibuni.” amesema

Ederson ameyasema hayo alipokuwa akitathmini mambo mbalimbali ndani ya klabu hiyo kwenye mahojiano mahsusi na City+ baada ya misimu 8 ndani ya klabu hiyo aliyoichezea michezo 361

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button