Kwingineko

Ed Sheeran aisaidia Ipswich kusajili, akutana na Taylor Swift

IPSWICH TOWN: MWANAMUZIKI Ed Sheeran ambaye ni mdau katika klabu ya mji wake wa Ipswich ameisaidia klabu hiyo kusajili mchezaji msimu huu wa joto.

Mtendaji Mkuu wa timu hiyo ametania kuwa mwanamuziki huyo ni sehemu ya timu ya kusajili wachezaji baada ya kusaidia kusajili mchezaji msimu huu kabla ya kupanda jukwaani na kutumbuiza na mwanamuziki mwingine, Taylor Swift.

Ashton alimtania Sheeran: “Ni sehemu rasmi ya timu yetu ya kuajiri”, akiongeza kuwa yeye ni “mtu wa ndani” na “gwiji wa kimataifa”.

Sheeran amekuwa mfadhili wa jezi za kilabu hiyo tangu 2021 na huonekana mara kwa mara kwenye mechi kwenye Uwanja wa Portman Road klabuni hapo.

Mark Ashton anadai kuwa mwigizaji huyo wa pop alipokea simu ya video ili kumhimiza mtu mpya anayetarajiwa kusaini mkataba wake wa kuhamia East Anglia.

Hakutaja jina la mchezaji huyo, lakini amesema:”Hakika anafunga mabao machache na ni shabiki wa Sheeran, ambaye ni mwanahisa mdogo katika klabu ya mji wake huo,

“Ed aliwasiliana na mchezaji huyo kwenye simu akiwa uwanja wa mazoezi, kabla hajapanda jukwaani na Taylor Swift,” Ashton aliambia hafla ya tasnia ya Soccerex huko Miami.

“Natumai hiyo ilikuwa sehemu muhimu katika kumfanya mchezaji kuvuka mstari na kuja kwetu.”

Sheeran na mwimbaji wa pop Swift walikuwa jukwaani pamoja Uwanja wa Wembley, siku moja kabla ya Sammie Szmodics kusajiliwa kutoka Blackburn.

Baada ya kufunga mkwaju wa juu katika ushindi wa 2-1 wa Ipswich dhidi ya Tottenham mwezi huu, alishiriki picha yake akiwa na Sheeran kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Ipswich itawakaribisha wababe Manchester United siku ya Jumapili, mechi ya kwanza ya mashindano kwa Ruben Amorim kuwaongoza Mashetani Wekundu.

Related Articles

Back to top button