Ligi Kuu

Dladla ataka Yanga iwe makini zaidi

DAR ES SALAAM: KAIMU Kocha Mkuu wa Yanga, Simon Dladla, amewataka wachezaji wake kuongeza makali na kufanya maamuzi sahihi wanapofika eneo la hatari ili wasipoteze nafasi zinazoweza kuamua matokeo.

Akizungumza Dar es Salaam baada ya mchezo dhidi ya Mashujaa jana, amesema licha ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 bado wanashindwa kutumia vizuri nafasi nyingi wanazotengeneza.

Dladla amesema kucheza nyumbani kunaiweka Yanga katika nafasi ya kuwajibika kupata matokeo, hivyo ni muhimu kwa wachezaji kuwa wakali mbele ya lango na kutumia vizuri nafasi wanazotengeneza.

Amesema benchi la ufundi linafahamu changamoto zinazoweza kujitokeza katika michezo ya ligi, lakini linaamini kikosi hicho kina uwezo wa kufanya maamuzi ya haraka na sahihi ili kufikia malengo yake.

Kocha huyo amesisitiza umuhimu wa wachezaji kuendelea kuboresha umakini katika eneo la mwisho la ushambuliaji, akieleza kuwa matumizi mazuri ya nafasi yanaweza kuwa tofauti kati ya ushindi na kupoteza pointi.

Ushindi huo umeendelea kuibakiza Yanga katika nafasi ya pili ikifikisha pointi 22 nyuma ya kinara Simba yenye pointi 24.

Related Articles

Back to top button