Omah Lay aumia mguu, asitisha ziara

LAGOS: STAA wa Nigeria, Omah Lay ametangaza kuahirisha ziara yake ya Clarity of Mind kutokana na kupata majeraha ya mguu.
Ziara yake hiyo ilitarajia kuanza kutimua vumbi Oktoba 30, mwaka huu lakini sasa itatangazwa ratiba nyingine baadae.
Kupitia ukurasa wake wa Mtandao wa X, Omah Lay alisema kwa sasa anatarajia kuuguza jeraha la ligament ya mguu wake kwa takriban wiki nne mpaka sita, kisha tarehe mpya za ziara hiyo zitatangazwa upya.
“Ninahuzunika sana kuwajulisha kuwa, kutokana na jeraha la ligament, tarehe zote za ziara ya Clarity of Mind kuanzia tarehe 30 Oktoba na kuendelea zimeahirishwa, ili nipate nafasi ya kupona katika kipindi cha wiki 4 hadi 6 zijazo.
“Taarifa kuhusu tarehe mpya na tiketi zitatolewa hivi karibuni. Asanteni kwa upendo wenu,” aliandika Omah Ley.
Ikumbukwe, wiki lliyopita Omah Lay aliripotiwa kuumia mguu wakati akijaribu kufanya sarakasi kwa ajili ya onesho lake, ambapo alikimbizwa hospitali huko Los Angeles.
Aidha, ziara hiyo ilihusisha nchi za Canada, New Zealand, Australia, Oman, Uturuki, Uswisi, Ubelgiji, Ujerumani, Italia, Ufaransa, Austria na nchi nyingine lukuki za Ulaya.



