Ligi KuuNyumbani

Ihefu katika mtihani tena leo

LIGI kuu ya soka Tanzania Bara inaendelea leo kwa michezo miwili kupigwa katika mikoa ya Arusha na Mbeya.

Ihefu inayoshika mkia nafasi ya 16 bila pointi baada ya kupoteza michezo yote 4 iliyocheza itakuwa mwenyeji wa Tanzania Prisons katika uwanja wake wa nyumbani, Highland Estates uliopo Mbarali.

Tanzania Prisons ipo nafasi ya 8 ikiwa na pointi 7 baada ya michezo 5.

Katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, Geita Gold itakuwa mgeni wa Polisi Tanzania.

Geita Gold ipo nafasi ya 13 ikiwa na pointi 3 baada ya michezo 5 wakati Polisi Tanzania inashika nafasi ya 14 ikiwa na pointi 2 baada ya michezo 4.

Oktoba 3 michezo miwili ya ligi hiyo imepigwa Dar es Salaam huku Yanga ikiifunga Ruvu Shooting kwa mabao 2-1 katika uwanja wa Benjamin Mkapa na Azam ikitoka kifua mbele dhidi Singida Big Stars kwa bao 1-0 katika uwanja wa Azam Complex.

Related Articles

Back to top button