Davido anapewa $300,000 na baba yake

LAGOS: MSANII maarufu wa muziki kutoka Nigeria, David Adeleke, ‘Davido’, amesema kwamba licha ya kuingiza mapato makubwa kupitia muziki wake, bado anapokea pesa kutoka kwa baba yake, bilionea Adedeji Adeleke.
Davido amesema kuwa baba yake hufanya hivyo kwa sababu bado ni mtoto wake. Katika maelezo yake, amesema:
‘Baba yangu bado ananipa pesa, mimi ni mtoto wake.
Alikuja kwenye onesho langu Uwanja wa State Farm Arena, na siku iliyofuata alinipigia simu na kunitumia $300,000 (takriban Tsh Milioni 780) kama kunipongeza.”
Maelezo haya yameibua mjadala miongoni mwa mashabiki na wafuasi wake kuhusu heshima na msaada unaoendelea kutoka kwa wazazi kwa watoto wao, hata baada ya kufanikisha kujitegemea kifedha.
Maoni yako ni yapi
Ni kawaida kwa baadhi ya familia tajiri kuendelea kuwasaidia watoto wao, hata wakiwa wakubwa, kama ishara ya heshima na mshikamano wa kifamilia.
Hata hivyo, baadhi ya watu wanaona kuwa ni muhimu watoto kujitegemea kwa muda fulani.
Katika kesi ya Davido, ni wazi kuwa msaada wa baba yake ni ishara ya upendo na pongezi kutokana na mafanikio yake.




