Ligi Kuu

Coastal Union: Fedha sio shida zetu

DAR ES SALAAM: KAIMU Kocha Mkuu wa Coastal Union, Joseph Lazaro amesema kupoteza mechi tatu za Ligi Kuu Bara ni sehemu ya mchezo na sio shida ya kifedha kwa wachezaji na benchi la ufundi.

Amesema hakuna shida ya mshahara kwa wachezaji hali iliyopelekea kupoteza michezo minne na kutoka sare na KMC FC bali haikuwa bahati kwao.

Coastal Union wamecheza michezo mitano kupoteza nne na sare mechi moja na kesho wanashuka dimbani kuwakaribisha Pamba jiji FC, Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi jijini.

Lazaro amesema mechi za nyuma haikuwa bahati kwao na hakuna matatizo ya mchezaji kudai mshahara wala shida yoyote na kesho wanaenda tofauti na mechi zilizopita.

“Tutaingia kivingine tunaenda kukutana na timu ambayo tunauwiano sawa, benchi la ufundi tumetulia na kufanyia kazi mapungufu yetu ikiwemo kuruhusu bao la mapema, washambuliaji kutotumia nafasi tunazotengeneza,” amesema Lazaro.

Ameongeza kuwa mchezo wa kesho wanaenda kushambulia zaidi ili kutafuta ushindi wa kwanza kwenye mchezo dhidi ya Pamba Jiji.

Related Articles

Back to top button