Clash of the Titans; Barcelona vs Bayern Munich
BARCELONA: Majabali ya Kijerumani Bayern Munich wapo jijini Barcelona kwa ajili ya mchezo wa raundi ya 3 ya ligi ya mabingwa barani Ulaya mchezo ambao unatazamiwa kuwa wa kusisimua zaidi hasa ukizingatia meneja wa sasa wa Barcelona Hansi Flick amewahi kuifundisha miamba hiyo ya Bavaria.
Rekodi zinaonesha Bayern kutawala michezo ambayo miamba hii imekutana ikiwa ni jumla ya michezo 11 ya hivi karibuni Bayern Munich imeshinda mechi 9 Barcelona ikishinda 2 na hakuna sare.
Kipigo kikubwa ikutanapo miamba hii kilikuwa Agosti 14, 2020 Barcelona ikikubali kisago cha mabao 8 – 2 nyumbani Camp Nou
katika mchezo wa robo fainali ya Ligi ya mabingwa barani Ulaya.
Mchezo huo utapigwa katika dimba la Estadi Olimpic Lluis Companys uliopo jijini Barcelona saa 4:00 usiku saa za Afrika Mashariki.
Pamoja na mechi hiyo michezo mingine ya UCL ni
Atalanta v Celtic (19:45)
Brest v Leverkusen (19:45)
Manchester City v Sparta Praha (22:00)
RB Leipzig v Liverpool (22:00)
Atlético Madrid v Lille (22:00)
Benfica v Feyenoord (22:00)
Salzburg v GNK Dinamo (22:00)
Young Boys v Inter (22:00)