Kwingineko

Christian Eriksen hana furaha Man United

Christian Eriksen amezumgumza na kocha Erik ten Hag kuelezea wasiwasi wake kuhusu kukosa muda wa kucheza Manchester United msimu huu.

Kiungo huyo wa kimataifa wa Denmark ameanza kucheza mechi 11 tu United huku 10 nyingine akitokea benchi.

Eriksen, 32, mchezaji wa zamani wa Tottenham na Inter Milan ni mmoja wa wachezaji wa masheteni hao wekundu wanaoathiriwa na uwepo wa Kobbie Mainoo.

“Siku zilizopita nilisema siridhishwi kwa kutocheza, lakini sio kitu kinachonifanya nikose usingizi, ” Eriksen ameuambia mtandao wa michezo wa tipsbladet.dk

Christian Eriksen alijiunga na Manchester United mwaka 2022.

Related Articles

Back to top button