Nyumbani

Chicharito atamani kuja kuwa kiongozi yanga

MTUNZA vifaa wa klabu ya Yanga, Godlisten Anderson maarufu ‘Chicharito’ amesema moja ya ndoto yake hapo baadaye ni kuja kuwa kiongozi wa klabu hiyo.

Akizungumza na SpotiLEO, Chicharito amesema kwa miaka kadhaa ambayo amekuwa sehemu ya timu hiyo, amejifunza na ataendelea kujifunza vitu vingi.

“Timu nimetoka nayo mbali, nina uchungu nayo, naamini nitakuwa mtu sahihi wa klabu yetu, kwasababu tayari nina uzoefu mkubwa nimekuwa nayo na nitazidi kuwa nayo,” amesema Chicharito.

Chicharito ambaye aliwahi kuwa mpiga picha wa klabu hiyo amesema mpaka sasa amejifunza masuala mengi ya kiuongozi ndani ya klabu hiyo.

“Kuna msimu bora kuna misimu inaumiza, kuna misimu ya kawaida, kutokana na hiyo mienendo na tabia hizo, natamani kufikia huko,” ameongeza Chicharito.

Related Articles

Back to top button