Mapinduzi CupNyumbani
Nusu fainali ya kisasi Mapinduzi Cup

NUSU fainali ya pili ya michuano ya Kombe la Mapinduzi inapigwa leo kati ya Singida Fountain Gate na Simba.
Mshindi wa mchezo huo kwenye uwanja wa New Amaan Complex atacheza fainali dhidi ya Mlandege iliyoitoa APR katika nusu fainali ya kwanza Januari 9.
Singida Fountain Gate itataka kulipiza kisasi cha kufungwa mabao 2-0 na Simba katika mchezo wa kundi B la michuano Januari 3.