MasumbwiMichezo Mingine

Mwakinyo afungua Milango kuzichapa na Kiduku

BONDIA Hassan Mwakinyo amemtaka ‘Mtoto’ wa Morogoro aendelee kumuomba pambano kwani kuna siku Dua yake itajibiwa.
Mwakinyo amedai lazima ajipange kwakuwa halitakuwa pambano la ‘Pesa ya Madafu’ kwani pambano hilo halitamuongezea Rank hivyo ni lazima avune pesa za kutosha.
”Sijaona Mpinzani wangu, kwa sababu sina ninachokitaka kwanza kutoka kwao labda kama wao wanacho wanachokitaka kutoka kwangu, pili ngumi ni mchezo ambao hautakiwi kumfagilia mtu, mpe mtu heshima lakini usiamini kama yeye ni bora kuliko wewe hicho kitu hakijaumbwa.”
“Tatu Boxer yoyote ambaye anania na mimi aendelee kuniomba kwa sababu hata huyu Mkenya alikuwa akiniimba sana lakini Mungu amejibu Dua yake, kuna siku pia huyu Mtoto wa Morogoro dua yake itajibiwa aendelee tu kuomba na Watu wa Morogoro waendelee kumswalia Mtume watajibiwa.
“Sio jambo kubwa kwa sababu sio maajabu ni kiasi cha kuamka tu nina akili mbaya nikaamua.”
Kwa muda mrefu sasa kumekuwa na majibizano ya hoja kati ya upande unaomsimamia bondia kutoka Morogoro Twaha Kassim maarufu Twaha Kiduku na bondia Hassan mwakinyo.
Mvutano huo umewafanya wadau wa Masumbwi kutamani pambano baina ya wawili hao licha ya kuonekana kuwa na ugumu lakini kauli za Mwakinyo zinafungua milango ya uwepo wa pambano hilo.

Related Articles

Back to top button