Bibi atamani kuwa Miss Universe akiwa na miaka 8
SEOUL, Korea Kusini: MWANAMITINDO wa Korea Kusini mwenye umri wa miaka 81, Choi Soon-hwa alishindwa katika azma yake ya kuwa mshiriki mwenye umri mkubwa zaidi wa Miss Universe baada ya kushiriki katika shindano la kitaifa la nchi hiyo dhidi ya wapinzani wenye umri wa kuwa wajukuu zake.
Bibi huyo licha ya kukosa la urembo lakini alitwaa tuzo ya ‘mvaaji bora’ katika shindano hilo.
Akiwa amevalia gauni jeupe lenye shanga, nywele zake za fedha alipanda jukwaani na kutumbuiza katika shindano la kuimba katika shindano la Miss Universe Korea lililofanyika katika mji mkuu wa Korea Kusini, Seoul.
Katika shindano hilo mwanamitindo Han Ariel, mwanafunzi wa shule ya mitindo mwenye umri wa miaka 22, alishinda shindano hilo na ataelekea Mexico City kwa shindano la 73 la Miss Universe litakalofanyika Novemba mwaka huu.
Choi, mfanyakazi wa zamani wa huduma ya hospitali ambaye alianza kazi yake ya uanamitindo katika miaka yake ya 70, alitangazwa kuwa mshiriki wa fainali ya Miss Universe Korea mapema mwezi huu pamoja na washiriki wengine 31.
“Hata katika umri huu, ninaujasiri wa kunyakua taji,” Choi aliambia The Associated Press saa chache kabla ya shindano hilo.
“Nataka watu waniangalie na watambue kuwa unaweza kuishi na afya njema na kupata furaha maishani unapopata mambo unayotaka kufanya na kujipa changamoto kufikia ndoto hiyo.”
Isingewezekana kwa Choi kushiriki katika shindano hilo mwaka mmoja uliopita kwani Miss Universe alikuwa amepunguza ushiriki wa wanawake wenye umri kati ya miaka 18 na 28. Kikomo cha umri kiliondolewa mwaka huu ikiwa ni sehemu ya jitihada za kulifanya shindano hilo kuwa la kisasa zaidi.
Waandaaji wa shindano la Kikorea pia waliondoa mashindano ya kuogelea na mahitaji ya kustahiki yanayohusiana na viwango vya elimu, urefu na uwezo wa lugha ya kigeni ili kufungua shindano hilo kwa wanawake zaidi.