Masumbwi

BFT, TPBRC kushirikiana kuboresha ngumi

DAR ES SALAAM: Viongozi waandamizi wa Shirikisho la Ngumi Tanzania (BFT) na Kamati ya muda ya Kamishemi ya Ngumi za kulipwa Tanzania (TPBRC) wamekutana Dar es salaam kuweka mikakati ya kushirikiana katika kuleta maendeleo ya mchezo wa ngumi nchini.

Kikao hicho cha awali kilifanyika katika ofisi za TPBRC jengo la NSSF Mafao, Ilala na kuhudhuriwa na Rais wa BFT Lukelo Willilo, Mwenyekiti wa kamati ya muda Emmanel Saleh na Makamu Mwenyekiti wake Alex Galinoma.

Willilo aliambatana pia na wajumbe wawili wa kamati ya utendaji Samwel Kapungu (Mwenyekiti wa kamati ya Semi-pro-boxing) na Mafuru Mafuru (Mwenyekiti wa kamati ya Waamuzi na Majaji).

Kwa mujibu wa Willilo, mikakati mikubwa iliyozungumziwa ni pamoja na kuweka mfumo thabiti wa mabondia wote kuanzia kucheza Ngumi za ridhaa ili kupata msingi mzuri wa mchezo wa Ngumi.

Pia, kuboresha mfumo wa kusimamia Afya na Usalama wa wachezaji ndani na nje ya ulingo kwa kutoa mafunzo mbalimbali kupitia madaktari mabingwa na kushirikiana katika kutoa mafuzo ya wataalamu wa mchezo wa Ngumi wakiwepo Waamuzi na Majaji, Walimu na Madaktari wa ulingoni katika ngazi za Kitaifa na Kimataifa.

Kamisheni imeahidi kutoa baadhi ya mabondia bora wa kike kushiriki michezo ya majaribio ya wanawake (Samia Women Boxing Championship) watakaoweza kuchaguliwa kujiunga na Timu ya Taifa ya wanawake kujiandaa na mashindano ya Ubigwa wa Dunia ya wanawake yatakayofanyika Nis, Serbia kuanzia Machi 6-17 2025.

Related Articles

Back to top button