Arteta awalilia Saka na Martinelli

LONDON:MENEJA wa Arsenal Mikel Arteta amesema anatumaini winga wake Bukayo Saka na mshambuliaji Gabriel Martinelli watarejea kikosini kutoka majeruhi wakati ambao washika mitutu hao wa jiji la London watakapowakaribisha Emirates majirani zao wa mji mmoja Fulham FC Aprili Mosi mwaka huu.
Kauli hii ya Arteta inakuja baada ya kosa kosa za wachezaji wake kuwagharimu pointi muhimu katika mbio za ubingwa kwenye mchezo dhidi ya Nottingham Forest jana Jumatano, pia wakati mgumu waliopata kusawazisha katika mchezo waliopoteza 1-0 mbele ya West Ham United Jumamosi iliyopita.
“Kesho tuna kikao kujadili maendeleo yao hasa Gabi (Gabriel Martinelli) ambaye nadhani ana nafasi nzuri ya kurejea kabla ya Bukayo, lakini ni haraka kiasi gani? Tutaona watakavyokuwa wiki ijayo au siku 10 zijazo lakini ni ukweli wa wazi nawahitajin kabla ya mchezo wetu dhidi ya Fulham” Arteta aliowaambia Wanahabari
Baada ya sare dhidi ya Nottingham Forest, Arsenal wanasalia nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi na point 54 point 13 nyuma ya vinara Liverpool wenye point 67 na sasa meneja huyo atahitaji kuhamishia nguvu zake kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya PSV Eindhoven Jumanne machi 4.