Tetesi

Arsenal yaitaka saini ya Ousmane Diomande

TETESI za usajili zinasema Arsenal imefikia ofa ya pauni mil 51 pamoja na bonasi iliyowasilishwa na Chelsea kumsajili beki wa Sporting Lisbon na Ivory Coast Ousmane Diomande, 20. (Record via Sun)

Tottenham ina nia kukamilisha dili la kudumu kwa ajili ya fowadi wa RB Leipzig na Ujerumani Timo Werner, 28, lakini haina haraka kuhuisha chaguo la kumnunua la pauni mil 14.5. (Four Four Two)

Manchester United inalenga kumteua kocha wa Brentford Thomas Frank kuchukua nafasi ya Erik ten Hag Old Trafford majira yajayo ya kingazi na sio kocha wa England, Gareth Southgate. (Football Transfers)

Hata hivyo, kwa mujibu wa ripoti nyingine mmiliki mwenza Sir Jim Ratcliffe na Ineos anapanga Ten Hag aendelee kuinoa United msimu ujao, lakini anaandaa mkakati wa kufanya mabadiliako haraka iwapo wataamua kumtimua. (inews)

Kiungo wa Aston Villa Nicolo Zaniolo anataka kurejea alikozaliwa, Italia toka klabu ya Galatasaray ya Uturuki wakati kipindi chake cha mkopo kitakapokwisha katika timu hiyo ya Ligi Kuu England. (Corriere dello Sport – in Italian)

Bayer Leverkusen ni miongoni mwa vilabu vya Ulaya vyenye nia kumsajili golikipa wa timu ya taifa ya England chini ya miaka 17 wa klabu ya Everton Douglas Lukjanciks, 16, majira yajayo ya kiangazi. (Mail)

Aston Villa na Everton zimeonesha nia kumsajili kiungo wa Barcelona na Hispania Fermin Lopez, 20.

Everton ilishindwa kumsajili mchezaji huyo wakati wa dirisha la uhamisho la Januari. (Sport)

Related Articles

Back to top button